KLABU ya Paris Saint-Germain imeibwaga 2-0 Rennes na kuendeleza kasi yao ya kukimbia taji la ubingwa wa Ligi Kuu Ufaransa.
Jeremy Menez alifunga bao la kwanza dakika ya 56 kwa PSG ambayo sasa inaongoza ligi kwa pointi saba zaidi. Zlatan Ibrahimovic alifunga la pili baada ya kazi nzuri ya David Beckham ambaye alikaribia kufunga bao lake la kwanza Ufaransa.
David Beckham akiupitisha mpira juu ya kipa Benoit Costil
Beckham akishangilia baada ya kazi yake nzuri kumaliziwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya mwisho, akiiwezesha PSG kushinda mechi ya kwanza Rennes tangu 2002.


.png)