KLABU ya Bayern Munich imetwaa taji lake la 23 la Bundesliga ikiwa imebakiza mechi sita kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt.
Kwa wiki kadhaa lilikuwa ni suaa tu la lini Bayern watatangazwa rasmi kuwa mabingwa wapya, wakiivua taji Borussia Dortmund na bao la Bastian Schweinsteiger dakika ya 53 limewapa wageni ushindi waliouhitaji.
Ushindi huo, unaifanya Bayern itimize pointi 75, 20 zaidi dhidi ya Borussia Dortmund walio katika nafasi ya pili, ambao wameifunga Augsburg 4-2.
Mshindi wa taji: Bao la Bastian Schweinsteiger lilitosha kuizamisha Eintracht Frankfurt
Maalum Frankfurt: Bastian Schweinsteiger akishangilia bao lake


.png)