MABAO mawili ya Tomas Rosicky yameipa Arsenal iliyokuwa pungufu ya mchezaji mmoja ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Brom katika Ligi Kuu ya England leo na kuziongezea presha Chelsea na Tottenham katika kinyang'anyiro cha nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Ushindi huo katika Uwanja wa The Hawthorns unaipandisha timu ya Arsene Wenger juu ya Chelsea katika nafasi ya nne wakizidiwa pointi moja tu na Spurs walio nafasi ya tatu na wapinzani wao hao wote wawili watakuwa kazini kesho.
Rosicky alikfunga mabao yake katika dakika za 20 na 50, wakati la wenyeji lilifungwa na kiungo James Morrison kwa penalti, baada ya Per Mertesacker kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumuangusha Shane Long.
Katika mchezo huo, kikosi cha West Brom kilikuwa: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Yacob, Brunt, Dorrans/Lukaku dk62), Morrison, Thomas/Rosenberg dk62 na Long.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Rosicky/Gibbs dk81, Ramsey, Gervinho/Vermaelen dk73, Cazorla/Coquelin dk89, Arteta na Giroud.
Nyota: Tomas Rosicky ameibeba Arsenal hadi nafasi ya nne kwa mabao yake leo
Bao la ufunguzi: Rosicky akiifungia Arsenal bao la kwanzaUwanja wa The Hawthorns...


.png)