|
Messi alicheza nusu ya mwisho ya kipindi cha Jumatano katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain licha ya kuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja na hakutarajiwa kucheza hadi mechi ya kwanza ya Nusu Fainali dhidi ya Bayern Munich, Aprili 23.
Busquets pia ameenguliwa kwenye kikosi hicho kwa sababu ya kuwa majeruhi, wakati Iniesta na Alba kuondolewa kwao ni maamuzi ya menejimenti.
Habari njema kwa Azulgrana ilikuwa ni kurejea mazoezini kwa Adriano leo na ameingizwa kwenye kikosi cha wachezaji 18 kinachokwenda Zaragoza.