• HABARI MPYA

    Saturday, April 13, 2013

    PODOLSKI MAMBO MAGUMU ARSENAL, AKERWA NA MAMBO MAWILI, BENCHI NA KUCHEZESHWA WINGI

    MUSTAKABALI wa Lukas Podolski ndani ya Arsenal uko shakani baada ya mshambuliaji huyo wa Ujerumani, kumaliza miezi miwili bila kuanza katika kikosi cha The Gunners.
    Arsenal imeshinda mechi zao sita kati ya saba zilizopita katika Ligi Kuu ya England na kocha Arsene Wenger anavutiwa kuwaanzisha Gervinho na Olivier Giroud katika safu ya ushambuliaji. 
    Out of favour: Podolski has lost his place in the Arsenal starting XI
    Mambo magumu: Podolski amepoteza nafasi kikosi cha kwanza Arsenal

    Podolski ni kama amepagawa na hali halisi ndani ya Arsenal na anataka apewe nafasi ya kuanza katika safu ya ushambuliaji. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 11 kutoka Cologne msimu uliopita, zaidi amekuwa akichezeshwa nafasi ya pembeni kushoto na Wenger, lakini angependa kucheza kama mshambuliaji wa kati. 
    Wing man: Podolski has been mainly used on the left by Wenger
    Winga: Podolski amekuwa akichezeshwa kama winga wa kuhsoto na Wenger

    Atletico Madrid na Juventus awali zilionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Bayern Munich, na sasa Galatasaray inafikiriwa kujiunga katika mbio za kuwania saini yake.
    Podolski - ambaye ameichezea mechi 108 nchi yake, Ujerumani- amefunga mabao 13 katika mechi 35 alizoichezea Arsenal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PODOLSKI MAMBO MAGUMU ARSENAL, AKERWA NA MAMBO MAWILI, BENCHI NA KUCHEZESHWA WINGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top