• HABARI MPYA

    Tuesday, April 02, 2013

    NIYONZIMA AWATULIZA ROHO MASHABIKI YANGA SC

    Haruna Niyonzima; Amrtuliza nafsi za mashabiki Yanga

    Na Mahmoud Zubeiry
    KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliofanya mazoezi na timu hiyo leo, Uwanja wa Kijitonyama, Dar es Salaam.
    Haruna alikosekana katika mchezo wa timu yake hiyo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Polisi mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kifamilia.
    Hali hiyo ilizua hofu kidogo kutokana na taarifa za baadhi ya magazeti nchini kwamba, kiungo huyo anataka kuhama.
    Lakini Niyonzima ametuliza roho za mashabiki wa Yanga baada ya leo kuibuka mazoezini kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Oljoro Aprili 10, mwaka huu.
    Yanga inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 49, baada ya kucheza mechi 21 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 43, Kagera Sugar 37 na Simba SC 34. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NIYONZIMA AWATULIZA ROHO MASHABIKI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top