• HABARI MPYA

    Monday, April 15, 2013

    REAL NA BARCA ZAUA 3-0, RONALDO ATIKISA MARA MBILI, KINDA LILILOCHUKUA NAFASI YA MESSI JANA NI HATARI, LAPIGA MBILI PIA


    NYOTA Mreno, Cristiano Ronaldo jana amefikisha mabao 50 katika mashindano yote msimu huu alipofunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiitandika 3-0 Athletic Bilbao katika La Liga.
    Ronaldo alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu dakika ya pili tu, hilo likiwa bao lake la 12 kufunga kwa mpira wa adhabu tangu asaini Real mwaka 2009.
    Akafunga tena kwa kichwa dakika ya 69 kufuatia krosi, kabla ya kutoa pasi kwa Gonzalo Higuain kufunga la tatu dakika saba baadaye.
    Thundering: Cristiano Ronaldo scores his side's second goal with a powerful header
    Mtu hatari: Cristiano Ronaldo akifunga bao lake la pili kwa kichwa

    Katika mechi nyingine, Radamel Falcao alifunga mabao mawili wakati Atletico Madrid ikiendelea na mbio za kuwania nafasi ya pil kwa kuitandika mabao 5-0 nyumbani Granada.
    Falcao, ambaye wiki hii imeelezwa atahamia Manchester United msimu ujao jana alifunga mabao yake katika dakika za 27 na 47 na kufikisha mabao 30 katika mashindano yote msimu huu.
    Diego Costa, Raul Garcia na Filipe Luis walifunga pia kwenye ushindi huo, vijana wa Diego Simeone wakishinda mechi ya 14 kati ya 16 za ligi kwenye Uwanja wa Vicente Calderon msimu huu.
    Ushindi huo, pia unaongeza presha kwa wapinzani wao wa Jiji la Madrid, Real, ambao wana pointi tatu zaidi zikiwa zimebaki mechi saba.
    Flying high: Ronaldo celebrates with Marcelo (left) during tonight's victory
    Anapaa kwa kasi: Ronaldo akishangilia na Marcelo (kushoto) usiku wa jana

    Nao vinara wa La Liga, Barcelona wameendeleza ubabe na kujisogeza jirani na ubingwa baada ya kuichapa mabao 3-0 Real Zaragoza jana, mshambuliaji Cristian Tello aliyechukua nafasi ya Lionel Messi akifunga mabao mawili. 
    Thiago Alcantara aliifungia bao la kuongoza Barcelona dakika ya 20 kabla ya kumtengenezea nafasi Tello kufunga la pili dakika ya 39. 
    Kinda huyo mwenye umri wa miaka, Tello akafunga la tatu dakika ya 53, tena kwa jitihada binafsi. 
    Young star: Tello marked his start with two goals to put pressure on Tito Vilanova that he deserves a starting berth
    Nyota Kinda: Tello ameanza na kufunga mabao mawili hivyo kumuonyesha Kocha Tito Vilanova kwamba anastahili namba kwenye kikosi cha kwanza

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: REAL NA BARCA ZAUA 3-0, RONALDO ATIKISA MARA MBILI, KINDA LILILOCHUKUA NAFASI YA MESSI JANA NI HATARI, LAPIGA MBILI PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top