Na PAUL COLLINS
|
KILELENI...
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amemaliza ukame wa mabao Manchester United akiiwezesha timu hiyo kupaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi 15 zaidi baada ya kuilaza Stoke City mabao 2-0.
Van Persie alikuwa amecheza mechi 10 za mashindano ya nyumbani bila kufunga, lakini leo amefunga bao la pili kwa penalti dakika ya 66, baada ya
Michael Carrick kufunga la kwanza dakika ya nne na sasa United inahitaji pointi saba tu katika mechi zake sita zilizobaki ili kuivua ubingwa Manchester City.
Katika mchezo wa leo vikosi vilikuwa; Stoke: Begovic, Cameron/Jerome dk71, Huth, Shawcross, Wilkinson, Shotton, Whelan, Nzonzi, Adam, Jones/Crouch dk84 na Walters/Owen dk77.
Manchester United: De Gea, Evra, Jones, Ferdinand, Vidic, Valencia, Carrick, Kagawa, Rooney, Hernandez/Welbeck dk77 na Van Persie.
Pati la ushindi: Wafungaji wa mabao ya United, Michael Carrick na Robin van Persie wakipongezwa na wenzao
Makocha: Tony Pulis kushoto wa Stoke na Sir Alex Ferguson kulai wa United leo
Katika mchezo mwingine, Sunderland iliichapa Newcastle mabao 3-0, lakini mashabiki 27 walikamtwa na Polisi watatu walijeruhiwa kufuatia vurugu zilizoibuka uwanjani.
Vurugu zilitokana na kundi la mashabiki wa Newcastle kujaribu kuwavamia mashabiki wa Sunderland baada ya kipigo Uwanja wa nyumbani, St James' Park.
Safari lupango: Shabiki wa Newcastle akisongeshwa na Polisi