• HABARI MPYA

    Monday, April 15, 2013

    VIGOGO WA BENKI WATEULIWA KWA JUKUMU ZITO YANGA SC

    Mwenyekiti wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la klabu ya Yanga, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam, Ridhiwani Kikwete kushoto akizungumza na Waandidhi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani. Kulia ni Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako. 

    Na Mahmoud Zubeiry
    MWENYEKITI wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam, Ridhiwani Jakaya Kikwete ameteua Wajumbe kadhaa wa kumsaidia kazi hiyo, wakiwemo wanasheria wawili na wataalamu wa Taasisi za Fedha.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika uteuzi wa Kamati hiyo, amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri na watu.
    Mtoto huyo wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema kwamba kutakuwa na Kamati mbili za kushughulikia mchakato huo, moja ikiwa ya wataalamu na nyingine ya watendaji.
    Aliwataja Wajumbe wa Kamati ya Wataalamu kuwa ni Makamu wake, Issa Hajji Ussi na Wajumbe Isaac Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, mtumishi ya Beki ya Uwekezaji Tanzania (T.I.B.),  Alan Magoma, Mwanasheria mkongwe, Mavale Msemo na mtumishi mwingine wa Benki, Charles Palapala.
    “Utaona kuna watu wengi wa taasisi za fedha, kwa sababu hili zoezi linahitaji fedha, tutaangalia kama tutaingia ubia na mtu, au sisi kama klabu tukawekeza kwenye mradi huo moja kwa moja,”alisema.
    Kwa upande wa watendaji, Kikwete alisema kwamba Kamati yao itaongozwa na Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako, Beda Tindwa na Mahmoud Milandu.
    “Kamati yetu sisi itakuwa ya kukaa na kutengeneza mipango na baadaye kama kutakuwa na barua ya kupeleka wapi, au mtu wa kufuatwa, basi ile kamati nyingine ndogo, itafanya kazi hiyo,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VIGOGO WA BENKI WATEULIWA KWA JUKUMU ZITO YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top