• HABARI MPYA

    Monday, April 15, 2013

    SIMBA NA AZAM ZAINGIZA MILIONI 66, YANGA NA OLJORO MILIONI 63

    Himid Mao kushoto na Amri Kiemba wakichuana katika mechi ya jana

    Na Boniface Wambura
    MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba uliochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza Sh. 66, 855, 000 kutokana na watazamaji 11,458.
    Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.
    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.
    Mchezo mwingine wa ligi hiyo, juzi kati ya Yanga SC na JKT Oljoro ulivutia watazamaji 11,021 na kuingiza Sh. 63,170,000.
    Viingilio katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.
    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA NA AZAM ZAINGIZA MILIONI 66, YANGA NA OLJORO MILIONI 63 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top