MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga SC katika mchezo wa leo yamefungwa na viungo mshambuliaji, Mganda Allan Jolly Okello mawili dakika ya 18 na 63 na Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 75.
Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 54 katika mchezo wa 22 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 46 za mechi 21, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 22 za mechi 22 pia nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16.
Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.



.png)
0 comments:
Post a Comment