• HABARI MPYA

    Sunday, May 10, 2026

    JKT TANZANIA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 MBWENI


    TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mzawa, Paschal Mussa Mambi dakika ya 60 na kwa ushindi huo JKT Tanzania wanafikisha pointi 35, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi moja na TRA United baada ya timu zote kucheza mechi 22.
    Kwa upande wao Mbeya City hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo wao wakibaki na pointi zake 21 za mechi 22 sasa nafasi ya 14 kwenye kigi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top