KLABU ya Wigan imetinga Fainali ya Kombe la FA kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga mabao 2-0 Millwall kwenye Uwanja wa Wembley jioni ya leo.
Mabao ya Shaun Maloney dakika ya 24 na Callum McManaman dakika ya 77 yanaifanya sasa Wigan isubiri mshindi kati ya Manchester City na Chelsea zitakazomenyana kesho, ikiwa ni miaka 35 tangu wachaguliwe kucheza Ligi.
Mashabiki wa Millwall waligombana wenyewe kwa wenyewe uwanjani leo.
Kikosi cha Millwall leo kilikuwa: Forde, Dunne, Shittu, Beevers, Lowry, Jack Smith/Hulse dk66, Abdou/Trotter dk72, St. Ledger, Henry, Keogh/Batt dk89 na Chris Taylor.
Wigan Athletic: Al Habsi, Beausejour/McArthur dk60, Alcaraz, Boyce, Figueroa, McManaman/Henriquez dk89, McCarthy, Scharner, Maloney, Kone na Gomez.
Shuti bao: Shaun Maloney akifunga baada ya kupokea pasi nzuri ya Arouna Kone
Shangwe: Wigan wakishangilia ushindi wao