KIUNGO Jack Wilshere amerejea, lakini iliwabidi Arsenal wafunge mabao matatu dakika za lala salama ili kurejea kwenye Nne Bora za Ligi Kuu ya England baada ya kuilaza mabao 3-1 Norwich kwenye Uwanja wa Emirates.
Huku Chelsea na Tottenham zikiwa hazichezi wikiendi hii kwa sababu ya Nusu Fainali ya Kombe la FA, The Gunners wana nafasi ya kurejesha matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Wageni walitangulia kupata bao kupitia kwa Michael Turner dakika ya 56, lakini Mikel Arteta akasawazisha kwa penalti dakika ya 85, kabla ya Bassong kujifunga dakika ya 88 kuipa Arsenal bao la pili na Lukas Podolski kuhitimisha ushindi kwa bao la dakika ya 90.
Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski, Sagna/Oxlade-Chamberlain dk80, Vermaelen, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere/Walcott dk59, Ramsey, Cazorla, Giroud na Gervinho/Podolski dk59.
Norwich: Bunn, Martin, Whittaker, Bassong, Turner, Johnson/Fox dk62, Snodgrass, Howson, Tettey/Jackson dk90, Holt na Kamara.
Kitu hicho: Mikel Arteta akiisawazishia bao Arsenal kwa penalti
Sheshe: Kipa Mark Bunn akimkoromea mshika kibendera baada ya kuwapa Arsenal penalti
Shangwe: Lukas Podolski akishangilia bao lake la dakika ya 90
Chukua hiyo: Michael Turner akifunga kwa kichwa