![]() |
Mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu akiwatoka mabeki wa JKT Oljoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. |
![]() |
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akimtoka kiungo wa JKT Oljoro, mbele ya refa Amon Paul |
![]() |
Mtaalamu; Haruna Niyonzima akijiandaa kupiga kona |
![]() |
Didier Kavumbangu akigombea mpira na beki wa JKT Oljoro |
![]() |
Hamisi Kiiza wa Yanga katikati akimtoka beki wa Oljoro kulia. Kushoto ni mshika kibendera namba moja, John Kanyenye akifuatilia mwenendo |
![]() |
Frank Domayo kulia akipenyeza mpira pembeni ya kiungo wa Oljoro, Hamis Saleh |
![]() |
Didier Kavumbangu akigombea mpira na beki wa Oljoro |
![]() |
Didier Kavumbangu akiwania mpira wa juu dhidi ya beki wa JKT Oljoro nyuma yake |
![]() |
Didier Kavumbangu akiwa amemuangukia kipa wa JKT Oljoro, Mussa Lucheke huku beki Nurdin Mohamed akiondoka na mpira |
![]() |
Sekeseke; Beki wa Oljoro akiwa hewani kupiga mpira wa kichwa wakati wa kizazaa langoni mwao |
![]() |
Hamisi Kiiza akikosa bao baada ya kipa Mussa Lucheke kuokoa mpira ambao hata hivyo ulimponyoka... |
![]() |
Hamisi Kiiza akijaribu kumpokonya mpira kipa wa Oljoro, Mussa Lucheke |
![]() |
Raha ya mechi bao; Simon Msuva akishangilia bao lake aliloifungia Yanga leo |
![]() |
Kipa wa JKT Oljoro, Mussa Lucheke akijaribu kupangua mpira wa juu bila mafanikio. Mpira ulimpita ukaokolewa na beki ukamkuta Nadir Haroub 'Cannavaro' akaukwamisha nyavuni kuipatia Yanga bao la kwanza |
![]() |
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya akimpatia huduma ya kwanza kiungo Athumani Iddi 'Chuji' mbele ya kocha Ernie Brandts kushoto |
![]() |
Kikosi cha Yanga leo |
![]() |
Kikosi cha JKT Oljoro leo |
![]() |
Simon Msuva akifumua shuti kufunga bao la pili la Yanga |
![]() |
Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza kushoto wakishangilia na Simon Msuva baada ya kufunga |
![]() |
Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' akiwa ameruka na kipa wa JKT Oljoro, Mussa Lucheke |
![]() |
Hamisi Kiiza akijiandaa kushangilia bao lake la tatu aliloifungia Yanga SC leo huku Mussa Lucheke akiushuhudia mpira (hauonekani pichani) unavyotinga nyavuni |
![]() |
Wachezaji wa Yanga Nadir Cannavaro, Haruna Niyonzima na Athumani Iddi wakimlalamikia refa Amon Paul kushoto |
![]() |
Kocha wa Yanga SC; Ernie Brandts akimpongeza Kiiza. Kulia ni Frank Domayo |
![]() |
Beki mkongwe wa Yanga SC, Nsajigwa Shadrack akimdhibiti mshambuliaji wa JKT Oljoro |
![]() |
Said Bahanuzi wa Yanga akifumua shuti pembeni ya Hamisi Kiiza na beki wa JKT Oljoro, Salim Mbonde, Bahanuzi alifunga, lakini refa akasema alikuwa ameotea kabla |