• HABARI MPYA

    Sunday, May 12, 2013

    AZAM FC WALIVYOJIHAKIKISHIA KUCHEZA TENA MICHUANO YA AFRIKA MWAKANI WAKIIWEKA BENCHI RASMI SIMBA SC HADI 2015

    IMEWEKWA MEI 12, 2013 SAA 2:40 USIKU
    Bao la 17; Kipre Herman Tchetche akijiandaa kupiga shuti kufunga bao la pili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Mgambo JKT jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Ushindi huo umeihakikishia Azam nafasi ya pili, itakayowawezesha kushiriki tena michuano ya Shirikisho Afrika mwakani, huku Tchetche akifikisha mabao 17 na kuzidi kuning'inia kileleni kwa ufungaji wa mabao kwenye ligi hiyo. 

    Mapacha; Kipre Michael Balou kulia akimpongeza pacha wake, Kipre Herman Tchetche kufunga bao

    Kipre Balou akichuana na kiungo wa Mgambo JKT

    Humphrey Mieno kushoto akichuana na kiungo wa Mgambo JKT

    Mashabiki wakijinafasi Uwanja wa Azam Complex

    Jamal Rwambow alikuwepo

    Beki wa Mgambo JKT akimdhibiti mshambuliaji wa Azam FC, Seif Abdallah

    Azam ina wenyewe; Mashabiki wa Azam wakishangilia soka safi na mabao leo

    Azam wera weraaaa; Simba wataisomaaa Afrika 2014...

    Wanachama waaminifu wa Azam

    Bin Zubeiry Family; Kutoka kulia Prince Akbar, Precious, mama yao Dina na Princess Asia wote walikuwepo Azam Complex leo 

    Jabir Aziz na Himid Mao leo walikuwa jukwaani

    Kipre Tchetche ni nomaaa!

    Kutoka kulia Sammih Hajji Nuhu, Khamis Mcha na Jackson Wandwi

    Kipre Tchetche anaambaa na mpira

    Beki wa Mgambo JKT akipitia mpira miguuni mwa Waziri Salum 

    John Bocco akimshuhudia kipa wa Mgambo JKT akidaka mpira

    Beki nwa Mgambo JKT akimdhibiti mshambuliaji wa Azam, Mganda Brian Umony

    Umony akipambana

    Daktari wa Mgambo JKT akimtibu kipa wake Tonny Kavishe

    Humphrey Mieno akimgeuza kiungo wa JKT Mgambo kwa chenga ambayo kama ungeiona live...unge...

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM FC WALIVYOJIHAKIKISHIA KUCHEZA TENA MICHUANO YA AFRIKA MWAKANI WAKIIWEKA BENCHI RASMI SIMBA SC HADI 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top