• HABARI MPYA

    Wednesday, May 08, 2013

    BARCA YATAKA KUBEBA KIPA WA LIVERPOOL PEPE REINA AKACHUKUE NAFASI YA VALDES

    MEI 8, 2013
    KLABU ya Barcelona iko tayari kumchukua kipa Pepe Reina wa Liverpool akachukue nafasi Victor Valdes mwishoni mwa msimu.
    Valencia inapiga danadana kutaja bei ya kipa wake namba moja, anayetakiwa na Barca, Vicente Guaita na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers hivi karibuni amesema hamuhesabii Reina katika mipango yake msimu ujao.
    Hiyo inamaanisha ofa kutoka Barcelona itakuwa mtihani kwa ahueni kwa klabu hiyo kupunguza gharama zake za mishahara.
    Reina ni kati ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa Liverpool na bado ana miaka mitatu katika mkataba wake, lakini ameamua kurejea kule ambako alianzia maisha ya soka.
    Wanted man: Pepe Reina could replace Victor Valdes at Barcelona
    Anayetakiwa: Pepe Reina anaweza kuziba 
    nafasi ya Victor Valdes Barcelona
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCA YATAKA KUBEBA KIPA WA LIVERPOOL PEPE REINA AKACHUKUE NAFASI YA VALDES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top