• HABARI MPYA

    Friday, May 10, 2013

    WACHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOYES MAN UNITED HAWA HAPA...

    IMEWEKWA MEI 10, 2013 SAA 4: 22 ASUBUHI
    KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes inasemekana anajiandaa kuwasajili wachezaji wa klabu yake ya zamani, Everton Marouane Fellaini na Leighton Baines aanze nao kazi katika klabu yake mpya akirithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
    Mscotland huyo mwenye umri wa miaka 50 aliteuliwa kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson Manchester United jana akisaini mkataba wa miaka sita na tayari anaweza kuwa anatazama wachezaji wapya wa kusajili.
    Kwa mujibu wa Daily Mirror, Moyes anatumai kuwahamishia Old Trafford, kiungo Mbelgiji Fellaini kama mbadala wa Wayne Rooney anayetaka kuondoka, na pia ana matumaini nyota wa England, Baines atafuatana naye.
    Dynamic duo: Leighton Baines (left) and Marouane Fellaini (right) could follow David Moyes out of Goodison
    Wanaondoka na kocha: Leighton Baines (kushoto) na Marouane Fellaini (kulia) wanaweza kumfuata David Moyes kuhama Goodison
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WACHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOYES MAN UNITED HAWA HAPA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top