• HABARI MPYA

    Friday, May 10, 2013

    KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013, NANI NI MSANII BORA WA KIUME, NANI WA KIKE?

    Ben Pol; Mmoja wa wanaowania tuzo ya Msanii Bora wa kiume

    Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 10, 2013 SAA 7:32 MCHANA
    ZOEZI la upigaji wa kura za tuzo za wanamuziki bora Tanzania, maarufu kama Kilimanjaro Music Award lililoanza Mei 2, mwaka huu linazidi kupamba moto kwa wapenzi wa muziki kuwapigia kura wasanii wawapendao.
    Jana kwa muhtasari tulielezea ushindani uliopo katika kipengele cha wimbo bora wa mwaka ambapo Rapa Kala Jeremiah, kupitia wimbo wake Dear God anachuana na kundi la Kigoma All Stars na wimbo wao Leka Dutigite, Mwasiti aliyemshirikisha Ally Nipishe katika wimbo Mapito, Ommy Dimpoz aliyemshirikisha Vanessa Mdee katika wimbo Me n U na Ben Pol katika wimbo Pete.
    Bado yumo; Lady Jaydee anawania tuzo ya Msanii Bora wa Kike

    Leo, tunahamia kwenye vipengele vya Msanii Bora wa Kiume na Msanii Bora wa Kike, ambacho kinawashindanisha Ben Pol, Diamond, Linex, Mzee Yussuf na Ommy Dimpoz kwa ‘wakaka’, wakati Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Lady Jaydee, Mwasiti na Recho watawania tuzo ya Msanii Bora wa Kike.
    Wasanii wote walioingia kuwania tuzo hizo ni ambao kwa hakika mwaka jana walitamba katika medani ya muziki nchini. Ni wasanii wanaobeba maana halisi ya Usanii bora- kutokana na kazi na wajihi wao.
    Hakika kuna ushindani mkubwa katika vipengele hivi na zaidi msanii atabebwa na idadi ya kura atakazopigiwa na mashabiki wake ili aweze kushinda tuzo hiyo. 
    Wapiga kura wanatakiwa kuandika namba ya msanii, wimbo, kikundi au bendi anayotaka ishinde na kisha kutuma kwenda namba 15346, wakati njia nyingine zaidi ya ujumbe mfupi (SMS) ni pamoja na Email, kwenda ktma@innovex.co.tz au kutembelea tovuti ya www.kilitimetz.com na kupiga kura moja kwa moja.
    Meneja wa Bia Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa tuzo hizo, George Kavishe aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba, wamejiandaa vizuri mwaka huu kuhakikisha zoezi linafana.
    Kilele cha sherehe za utoaji tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards zilizobeba kaulimbiu ya Kikwetu kwetu ni Juni 8, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, ambako pamoja na wasanii mbalimbali kupokea tuzo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali pia. 
    Je, katika Msanii Bora wa Kike na wa Kiume, utampa nani na nani kura zako?
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KUELEKEA TUZO ZA KILI KIKWETUKWETU 2013, NANI NI MSANII BORA WA KIUME, NANI WA KIKE? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top