• HABARI MPYA

    Tuesday, July 09, 2013

    ARSENAL SASA NJIA NYEUPE KUMNASA SUAREZ, AWAAMBA LIVERPOOL ANATAKA KUCHEZEA LIGI YA MABINGWA

    Na Martine Blackburn, The Sun, IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 4:30 ASUBUHI 
    HATIMAYE Luis Suarez ametaja sababu halisi ya kumfanya atake kuondoka Liverpool — ni kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa. Mshambuliaji huyo awali alisema katika mahojiano na Televisheni ya Uruguay kwamba alitaka kuondoka kuandamwa na vyombo vya Habari England na adhabu kali za FA kwa kumtuhumu kumfanyia hila za ubaguzi beki wa Manchester United, Patrice Evra na kumng’ata Branislav Ivanovic wa Chelsea. 
    Anaenda Arsenal? Suarez anataka
    kucheza Ligi ya Mabingwa

    Lakini wakala wake, Pere Guardiola amekutana na kocha wa Wekundu hao, Brendan Rodgers na Mkurugenzi Mkuu, Ian Ayre kwenye viwanja vya mazoezi vya Melwood jana na kusema kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya imekuwa sababu kubwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutaka kuondoka. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema yuko tayari kutoa Pauni Milioni 30 kwa ajili ya Suarez, lakini Kop wamemuambia zitahitajika Pauni Milioni 40 ili kukaa mezani kuzungumzia dili hilo. Real Madrid pia inamtaka Suarez.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL SASA NJIA NYEUPE KUMNASA SUAREZ, AWAAMBA LIVERPOOL ANATAKA KUCHEZEA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top