• HABARI MPYA

    Tuesday, July 09, 2013

    AZAM WAYAFUMUA MAJESHI YOTE YA JKT TANZANIA..WAYAPIGA 1-0 TAIFA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 12:45 JIONI
    BAO pekee la beki Luckson Kakolaki dakika ya 33, leo limeipa ushindi wa 1-0 Azam FC katika mchezo wa kirafiki dhidi ya kombini ya timu za Majeshi ya Kujenga Taifa (JKT) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Shujaa wa leo; Luckson Kakolaki amefunga baio pekee leo Azam ikiizamisha JKT

    Bao hilo lilitokana na kona maridadi iliyochongwa na beki Malika Philip Ndeule na kusababisha kizazaa langoni mwa JKT kabla ya Kakolaki kuuotea mpira na kuutumbukiza nyavuni.
    Mchezo huo ulikuwa maalum kuazimisha sherehe za miaka ya JKT na wachezaji wa timu za jeshi hilo za Ligi Kuu, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, JKT Mgambo na JKT Oljoro waliunagana kupambana na washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita.
    Azam iko katika maandalizi ya msimu mpya, na wiki mbili za mwanzo za mwezi ujao watakwenda Afrika Kusini kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga SC.
    Wakiwa huko, Azam pamoja na kufanya mazoezi katika viwanja vizuri, pia watapata mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu za Ligi Kuu za huko, zikiwemo Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns.
       
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM WAYAFUMUA MAJESHI YOTE YA JKT TANZANIA..WAYAPIGA 1-0 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top