IMEWEKWA JULAI 12, 2013 SAA 12:43 ASUBUHI
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ambaye mambo hayamuwndei sawa kwa sasa, amelazimika kurejea nyumbani kutoka kwenye ziara ya Manchester United kujiandaa na msimu mpya – siku moja tu tangu wachezaji 200 na viongozi watue Bangkok kwa ajili ya mechi ya kwanza ya ziara hiyo.
Mshambuliaji huyo wa England, ambaye kwa kiasi kikubwa amekuwa akihusishwa na kuondoka klabu hiyo majira haya ya joto, amemumia nyama za paja.
Rooney amesema katika Facebook: "Nasikitika nimeumia nyama za paja wakati mazoezi yalikuwa yanaendelea vizuri, narejea Manchester kwa ajili ya matibabu na hakuna cha kuhofia juu ya hili,".
Maumivu: Wayne Rooney (kulia) akiwa ametulia na Patrice Evra kabla ya kurejea nyumbani England
Mikosi: Rooney (kushoto) aliwasili Bangkok, lakini anarejea nyumbani mara moja kwa matibabu
Taarifa imesema: "Kufuatia vipimo jioni hii juu ya maumivu ya nyama mazoezini, imeamuliwa kwamba Wayne Rooney atarejea nyumbani mara moja kwa matibabu na uangalizi zaidi. Matarajio atakuwa nje ya Uwanja kwa mwezi mmoja.'
Rooney atatumia kiasi cha wiki mbili na nusu akifanya mazoezi ya peke yake chini ya maofisa wa tiba wa United katika viwanja vya mazoezi vya Carrington baada ya kuumia nyama za paka dakika kadhaa katika awamu ya kwanza ya mazoezi Thailand,".
Sasa atapambana kuhakikisha anakuwa fiti kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano wa United, wakianza na mabingwa wa Kombe la FA, Wigan katika Ngao ya Jamii Uwanja wa Wembley, Agosti 11.