• HABARI MPYA

    Friday, July 12, 2013

    MOYES SASA AMJIA JUU MOURINHO...AMCHANA KINOMA KUHUSU KUMTONGOZA HADHARANI ROONEY

    IMEWEKWA JULAI 12, 2013 SAA 11:17 JIONI
    KOCHA wa Manchester United, David Moyes amejibu maneno ya Jose Mourinho kuhusu Wayne Rooney kwa kusema msistizo kwamba, mshambuliaji huyo wa England hauzwi.
    Moyes amesema hayo katika Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari kwenye ziara ya Asia na Australia mjini Bangkok, Uwanja wa Rajamangala leo mchana, kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya Singha All Stars kesho .
    Maswali kibao yaliibuka kuhusu Rooney, ambaye amerejea nyumbani kutoka kwenye ziara hiyo baada ya kuumia nyama.
    Direct approach: Jose Mourinho has admitted he likes Wayne Rooney 'very much'
    Kutongoza moja kwa moja: Jose Mourinho amesema anampenda Wayne Rooney 'ile mbaya'

    Mapema leo, kocha wa Chelsea, Mourinho amezungumzia namna anavyomzimikia Rooney, akifanya hivyo mara ya pili tangu arejee Stamford Bridge majira haya ya joto.
    Alipoulizwa juu ya hilo, Moyes alisema: "Labda iwe  nilizungumza Kiholanzi wiki iliyopita, tumesema Wayne Rooney hauzwi.
    "Watu wanapenda kuzungumzia wachezaji wazuri. Napata maswali mengi kuhusu Wayne. Jose amekuwa akiulizia wachezaji pia. Ni vigumu kwangu kurudia rudia, lakini nitafanya hivyo - Wayne ni mchezaji wa Manchester United na itabakia kuwa hivyo'.
    Sent home: Wayne Rooney has left United's tour of Thailand with a hamstring injury
    Amerudishwa nyumbani: Wayne Rooney ameondoka kwenye ziara ya United, Thailand baada ya kuumia nyama
    Respectful: Jose Mourinho, Frank Lampard, Eden Hazard and more have arrived in Bangkok
    Heshima: Jose Mourinho, Frank Lampard, Eden Hazard na wengine wa Chelsea wamewasili Bangkok
    The Special One: The fans have made no secret about who their main attraction is
    The Special One: Mashabiki wakionyesha hisia zao wazi wazi
    In the shade? Mourinho's rarely known for taking a back seat
    Mourinho anapenda kukaa siti ya nyuma
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOYES SASA AMJIA JUU MOURINHO...AMCHANA KINOMA KUHUSU KUMTONGOZA HADHARANI ROONEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top