IMEWEKWA JULAI 12, 2013 SAA 11:36 JIONI
OMBI la Arsenal kumsajili mshambuliaji, Real Madrid Gonzalo Higuain limekutana na kizingiti kingine baada ya taarifa nchini Hispania kusema kwamba mshambuliaji huyo sasa anajisikia kubaki.
Kulikuwa kuna taarifa tofauti kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa mika 25 alitarajiwa kuwasili London, kwa ajili ya mipango ya uhamisho wa Pauni Milioni 23 ikifirikiwa makubaliano yalifikiwa wiki mbili zilizopita.
Rais wa Madrid, Florentino Perez ameyapuuzia madai hayo na gazeti la Marca la Hispania limesema Muargentina huyo atakutana naye Jumatatu kwa mazungumzo.
Anjiandaa kubaki: Kigeugeu cha Higuain na Real hakika kinawachanganya mashabiki wa Gunners
Timu hiyo ya Hispania inaanza maandalizi ya msimu mpya Jumatatu na sasa inatarajiwa kwamba Higuain atabakia huko, tayari kucheza mechi za mwanzoni za kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Bournemouth, Lyon, na Paris Saint-Germain.
Higuain alionyesha nia yake ya kuondoka Madrid mwishoni mwa msimu uliopita, wakati huo timu ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Lakini sasa inaonekana atakuwa katika mipango ya kocha mpya, Carlo Ancelotti, hususan kutokana na ukweli kwamba hakuna ombi rasmi la kumsajili lililowasilishwa na Arsenal au mwingine yoyote.
"Hatutaki aondoke. Zaidi ya hapo, hakuna yeyote kutoka Arsenal ametoa aina yoyote ya ofa, si kwa Euro Milioni 27, au chochote," Perez aliliambia gazeti hilo la Hispania.
Mwanzo mpya: Mshambuliaji huyo anaweza kuwamo katika mipango ya Ancelotti msimu huu
Walengwa wapya: Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez (kushoto) na wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia) wanatakiwa Arsenal
Inafikiriwa sasa Wenger amehamishia ndoana zake kwa mshambuliaji kinda wa miaka 20, Mfaransa Yaya Sanogo.
The Gunners pia imetangaza ofa kwa mshambuliaji mtata wa Liverpool, Luis Suarez, na alipoulizwa kama amepanda dau la Pauni Milioni 40 kumnasa nyota huyo wa Uruguay, Wenger alisema kidogo.
Wakati huo huo, kocha David Moyes ameendelea kushikilia msimamo wake kwamba Wayne Rooney atabakia Manchester United- maana yake hilo ni pigo pia kwa Arsenal.