IMEWEKWA JULAI 12, 2013 SAA 3:53 USIKU
MPENZI wa zamani wa Mario Balotelli na mama wa mtoto wake wa kike, amewafungulia mashitaka wazazi wa mwansoka huyo baada ya kuandika barua ya wazi wakimshutumu kujinufaisha kifedha na matanuzi kwa mtoto wao.
Kimwana huyo wa shoo, Raffaella Fico, mwenye umri wa miaka 25, na Balotelli, mwenye miaka 22, walikuwa katima dimbwi zito la mahaba lililomalizika mwishni mwa msimu uliopita, kabla haijajulikana alikuwa mja mzito wa binti yao, Pia, aliyezaliwa Desemba. Lakini Balotelli amemkataa mtoto hadi kwanza wafanye vipimo vya DNA ili ajiridhishe kwamba yeye ni baba wa mtoto.
Tangu hapo, wawili hao wamekuwa katika vita ya maneno kupitia magazeti na majarida mbalimbali na Raffaella amekuwa akimtuhumu kutokakuwa na haja na mtoto, ambayo imesababisha pia na wazazi wake waliomuasili, Franco na Silvia Balotelli kuingilia kati kwa kusema; "Mapenzi hayo yalikuwa zaidi kwa ajili ya fedha na umaarufu,".
Walisema: "Mtoto wetu wa kiume si wa sawa yako wala wa hadhi yako (Raffaella). Kwa muda fulani umekuwa ukizungumza katika umma, kwa Waandishi wa Habari, kwa wapiga picha,".
Tatizo: Ni wakati mwingine asiotaka Balotelli ambao anakabiliana nao sasa
Na matokeo ya habari hiyo katika gazeti la kila siku linaloongoza kwa muzo Italia, Gazzetta Dello Sport, mwanamitindo huyo wa vichupi, ambaye pia amekuwa akihusishwa kuwa katika mapenzi na Cristiano Ronaldo, amefungua kesi dhidi yao katika Mahakama ya Milan.
Katika taarifa iliyoandika kama sehemu ya malalamiko yake, Raffaella, amesema: "Katika barua yao ya wazi wamesema nilivutiwa tu na umaarufu na fedha, lakini Mario na mimi tulikuwa tuna uhusiano ambao uliisha Aprili 2012. .Ilikuwa tamu na hadithi ya kupendeza ya mapenzi ambayo ilitupa mtoto wa kike, Pia.'
'Furahia jua kali': Mpenzi wa zamani wa Balotelli, Raffaella Fico ameposti picha hii kwenye ukurasa wake wa twitter
Mashitaka haya yanaweza kuwagharimu walalamikiwa malefu ya mamia ya Euro, lakini bado tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo haijatajwa na haijulikani kama Balotelli atahitajika kutoa maelezo.
Raffaella na Balotelli, ambaye aliondoka Manchester City Januari kuhamia AC Milan, walitengana baada ya kusoma juu ya mwanasoka huyo kuwa dhaifu kwa wanawake na akaenda Uingereza kumvaa katika nyumba aliyokuwa akiishi, Cheshire, lakini mshambuliaji huyo alikataa kuonana naye na Polisi wakaitwa.
Kabinti Pia kalizaliwa Desemba na Balotelli hajawahi hata kukaona, licha ya Raffaella kumtaka afanye hivyo lakini amekuwa akikataa na akiendelea kusistiza vipimo kwanza.
Mpenzi mpya: Mpenzi mpya wa Balotelli, Fanny Neguesha (juu) na chini, jezi za timu ya taifa ya Italia za wawili hao
Tangu wakati huo, amepata mpenzi mpya, mwanamitindo, Fanny Neguesha na ameposti picha yao ya pamoja kwenye Twitter na kuonyesha jezi zao za zenye majina yao nyuma na pia amemvalisha pete ya uchumba ya almasi yenye thamani ya Pauni 100,000.
Raffaella amejibu mapigo kwa kuposti picha yake akiwa anapigwa jua kabaa kibikini kuelekea sherehe ya ubatizo ya mwanawe, Pia Jumapili katika kanisa lililo jirani na nyumbani kwao, Naples.