• HABARI MPYA

    Saturday, July 13, 2013

    BILIONEA WA MAREKANI MWENYE ASILI YA INDIA AINUNUA FULHAM

    TAJIRI Mohamed Al Fayed amethibitisha kuiuza klabu ya Fulham kwa vilionea wa Kimarekani, Shahid Khan, ambaye tayari anamiliki timu ya NFL, Jacksonville Jaguars.
    Uhamishwaji umethibitishwa na Ligi Kuu ya England. Khan anamiliki asilimia 100 ya hisa za klabu sasa na hakuna deni. Tangazo rasmi linatarajiwa kutolewa saa 7 mchana wa leo Craven Cottage.
    "Wakati wa kuwa mmiliki wa Fulham Football Club siku moja utafika mwisho, na nafikiri wakati huo sasa umefika,"alisema Al Fayed.
    In talks: Jacksonville Jaguars owner Shahid Khan is in talks to buy Fulham
    Mazungumzo: Mmiliki wa Jacksonville Jaguars, Shahid Khan akizungumzia kuinunua Fulham

    TOFAUTI YAO...


    AL FAYEDKHAN
    UMRIMiaka 84Miaka 62
    KUZALIWAAlexandria, MisriLahore, Pakistan
    UTAJIRIPauni Milioni 872Pauni Bilioni 1.7 (2012)
    BIASHARA ZAOFulham FC, Ritz Hotel, Paris, Balnagowan Castle & Estates, CocosaFlex-N-Gate na Jacksonville Jaguars
    "Wakati ni mwafaka kwa sababu nimempata mtu mzuri sana wa kuichukua, Shahid Khan amekubali kupokea majukumu na kipaumbele ambacho nimekuwa nacho Fulham tangu mwaka 1997. 
    "Fulham itakuwa katika mikono mizuri sana na Shahid, ambaye ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na mwenye mapenzi na michezo kwa kila ushahidi. Naomba kila mmoja anayependa Fulham na Uwanja wetu wa nyumbani wa Craven Cottage kumkaribisha Shahid kuanza safari yake ya kuwa mlezi mpya wa Fulham Football Club,"alisema.
    Khan alisema:  "Nimekuwa mwenye bahati sana hivi karibuni, kutambulishwa na Mohamed Al Fayed, mtu ninayemuheshimu na kumzimikia kwa mambo aliyoyafanya katika maisha yake na - juu ya yote, kwa aliyowafanyia wengine,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BILIONEA WA MAREKANI MWENYE ASILI YA INDIA AINUNUA FULHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top