• HABARI MPYA

    Saturday, July 13, 2013

    WENGER AANZA MAZUNGUMZO YA KUONGEZA MKATABA MPYA ARSENAL...AWAKANA PSG KINOMANOMA

    IMEWEKWA JULAI 13, 2013 SAA 1:13 ASUBUHI
    KOCHA Arsene Wenger yu mbioni kurefusha muda wake wa kuendelea kufanya kazi Arsenal, baada ya kugundulika ameanza mazungumzo ya Mkataba mpya na klabu.
    Mkataba wa sasa wa Mfaransa huyo unaisha majira yajayo ya joto, na ikazua tetesi huenda huo ukawa mwisho wake wa kufanya kazi katika klabu hiyo.
    Lakini Wenger amesema nia yake ni kuongeza Mkataba wa mshahara wa Pauni Milioni 7.5 kwa msimu na mazungumzo ya awali na Mtendaji Mkuu wa klabu, Ivan Gazidis yanaendelea.
    Signing on: Arsene Wenger is set to seal a new deal at the Emirates and snub suitors PSG
    Saini hapa: Arsene Wenger anajiandaa kusaini Mkataba mpya Emirates na kuzima ndoto za kuhamia PSG
    Signing on: Arsene Wenger is set to seal a new deal at the Emirates and snub suitors PSG
    Staying put: Arsene Wenger (left) will stay at Arsenal after admitting talks over a new deal have begun
    Anabaki: Arsene Wenger (kushoto) atabaki Arsenal baada ya kusema mazungumzo ya Mkataba mpya yameanza.
    Lads on tour: Jack Wilshere and his Arsenal team-mates arrived in Indonesia to start the pre-season tour
    Jack Wilshere na wachezaji wenzake wa Arsenal wamewasili Indonesia kuanza ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya
    Men of many talents: Alex Oxlade-Chamberlain showed his skills on the piano
    Vipaji vilivyojificha: Alex Oxlade-Chamberlain (juu) na Wojciech Szczesny wakionyesha vuipaji vyao vya kupiga piano 
    Men of many talents: Wojciech Szczesny showed his skills on the piano
    "Kuhusishwa na PSG kupo kwa sababu mimi ni Mfaransa na ninawajua wamiliki. Lakini kama hiyo ndiyo sababu ningekuwa huko tayari.
    "Moyo wangu upo na Arsenal. Mimi si PSG kwa sababu moyo wangu upo na Arsenal,"alisema. 
    Wenger amewasili Indonesia jana kwa ajili ya mechi ya kwanza ya ziara ya Arsenal Mashariki ya Mbali akiwa na mshambuliaji kinda wa miaka 20, Mfaransa Yaya Sanogo, kutoka Auxerre, mchezaji pekee aliyemsajili hadi sasa majira haya ya joto.
    Baada ya miaka kadhaa ya ubakhili, The Gunners itakuwa tayari kubomoa benki sasa kusajili japo mchezaji mmoja wa bei kubwa.
    Wenger anaweza kufanikisha usajili wa Pauni Milioni 23 wa mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain, wakati klabu hiyo pia inawataka Wayne Rooney na Luis Suarez.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WENGER AANZA MAZUNGUMZO YA KUONGEZA MKATABA MPYA ARSENAL...AWAKANA PSG KINOMANOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top