Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 5:20 ASUBUHI
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) asubuhi ya leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu za SImba na Yanga SC, vyenye jumla ya thamani ya Sh. Milioni 80, yaani Sh. Milioni 40 kila klabu.
TBL imekuwa ikizidhamimi klabu hizo kongwe nchini tangu mwaka 2008, kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager na leo Meneja wa kinywaji hicho, George Kavishe alikabidhi vifaa hivyo katika ukumbi wa Kili Pub Roots, Masaki, Dar es Salaam.
Makatibu wa klabu hizo, Evodius Mtawala wa Simba na Lawrence Mwalusako wa Yanga SC walipokea vifaa hivyo na kutoa shukrani kwa TBL kwa kuendelea kutekeleza vyema vipengele vya Mkataba.
Kavishe amesema katika Mkutano huo kwamba ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imekabidhi vifaa vya michezo kwa klabu hizo ajili ya msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
“Tunawapatia vifaa mapema kabla ya ligi kuanza ili wapate muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya msimu wa 2013/14 ambayo bila shaka itakuwa na changamoto kubwa kwa timu hizi mbili na pia tunaamini kuwa siri ya mafanikio katika michezo ni maandalizi mazuri.
“Ni matumaini yetu kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa Simba na Yanga wataiwakilisha Kili vizuri na kufurahia kuzichezea klabu hizi kongwe,”alisema Kavishe leo kuwaambia Waandishi wa Habari.
Kavishe aliongeza kuwa vifaa ambavyo ametoa leo ni pamoja na mipira, viatu, soksi, vizuia ugoko, jezi za mazoezi, jezi za mechi, glavu na vitu vya kuchezea mpira na kukimbilia na kusafiria, ambavyo anaamini vitaziwezesha timu hizo kucheza wakifurahia kuvaa vifaa vyenye ubora wa hali ya juu.
“Kilimanjaro Premium Lager kama mdhamini mkuu wa Simba na Yanga, na kinywaji kinachoongoza katika udhamini wa soka hapa nchini tunadhani kwamba uhusiano wetu na klabu hizi ni kiungo muhimu sana katika kuendeleza mpira wa miguu hapa Tanzania,”. “Tutaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi na kama ilvyo kawaida yetu, tutahakikisha tunalifikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,”.
Kavishe alisema kuwa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Simba na Yanga umelenga kukuza soka la Tanzania, kuleta msisimko, na kuvutia mashabiki wengi wa mpira wakati na vilevile kuwaweka wachezaji wa Tanzania katika nafasi nzuri ya kimataifa.
“Tunawashukuru viongozi wa Simba na Yanga, mashabiki wote, vyombo vya habari na wadau wote wa mpira kwa ushirikiano mzuri tunaoendelea kupata kwenye udhamini wetu na hiyo ndio siri ya mafanikio ya uhusiano wetu na klabu hizi mbili maarufu,”alisema.
“Tunawaomba mashabiki wa Simba na Yanga waendelee kuiunga mkono bia yao ya Kilimanjaro Premium Lager kwani tunafanya kila jitihada kuwapa burudani na kufikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,”alisema.

![]() |
| Kavishe akimkabidhi jezi Mwalusako |
![]() |
| Kavishe akimkabidhi Mtawala |
![]() |
| Kavishe mezani na Mwalusako na Mtawala |

.png)