IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 11:14 ALFAJIRI
KLABU ya Chelsea itampa Wayne Rooney mshahara wa Pauni 240,000 kwa wiki katika Mkataba wa miaka mitano dili ambalo litamfanya akunje Pauni Milioni 60, kama atalazimisha kuondoka Manchester United.
Rooney ni chaguo la kwanza la Jose Mourinho katika usajili wa sasa na bosi huyo wa Chelsea ameendelea kuwa na matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo majira haya joto.
Pamoja na kwamba Rooney aliambiwa na David Moyes wiki iliyopita kwamba hataruhusiwa kuondoka United, kuna mambo ambayo hayajatatatuliwa.
Mlengwa: Chelsea inataka kuomba kumsajili Wayne Rooney licha ya David Moyes kusema hauzwi
Atabaki au ataondoka? Mustakabali wa Rooney Manchester United umekuwa haueleweki majira haya ya joto
Mtu mpya kazini: David Moyes amesema kwamba hataki kumuuza Rooney
Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake Old Trafford, hajaonyesha dalili za kugeuza mawazo yake na Chelsea inataka kutumia nafasi hiyo.
Atawagharimu kama Pauni Milioni 30 kama United watakubali kumuuza, lakini hiyo haitakuwa ngumu kwa Chelsea.
Mourinho, ambaye alianza kuinoa timu hiyo jana baada ya kurejea tena majira haya ya joto, anataka kumpa Rooney mwanzo mzuri Stamford Bridge.
Mourinho pia anafuatilia nafasu ya Luis Suarez Liverpool na amewataka washauri wake kuendelea kumfahamisha juu ya nafasi yake. Arsenal pia inamfuatili mshambuliaji huyo wa Uruguay, lakini inabaki kuelekeza nguvu zake zaidi kwa Gonzalo Higuain kutoka Real Madrid.
Higuain amekubali kujiunga na The Gunners katika dili ambalo litamfanya Muargentina huyo akunje mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Lakini klabu hizo bado zinapingana kwa kiasi cha Pauni Milioni Milioni 2 katika ada ya uhamisho wake— na Real inataka Pauni Milioni 25.


.png)