• HABARI MPYA

    Tuesday, July 09, 2013

    BARCELONA YAMTENGEA PAUNI MILIONI 30 DAVID LUIZ, LAKINI CHELSEA...

    IMEWEKWA JULAI 9, 2013 SAA 10:59 ALFAJIRI
    KLABU ya Barcelona imetangaza ofa ya Pauni Milioni 30 kwa ajili ya beki David Luiz – lakini Chelsea itagoma kumuuza kwa bei hiyo.
    Barca, ambao pamoja na ubora wao wote, wana hasara katika safu ya ulinzi, wanatarajiwa kuboresha ofa hiyo kwa ajili ya beki huyo mwenye kipaji ambao wanataka awe mbadala wa Nahodha wao, Carles Puyol.
    Vyanzo vimesema ni 50/50 kwaLuiz kubaki Chelsea, ambako amekuwa mchezaji tegemeo tangu awasili Januari mwaka 2011 akitokea Benfica, au kuhamia kwa timu hiyo kubwa Ulaya.
    Highly rated: David Luiz is among the best defenders in the Premier League
    Thamani ya juu: David Luiz ni miongoni mwa mabeki bora katika Ligi Kuu England
    Gerard Pique
    Brazil's Neymar
    Wanamsubiri: Luiz anaweza kucheza pamoja na Gerard Pique na Neymar Camp Nou

    Pamoja na uwezekano wa kuungana na Gerard Pique au Puyol katika safu ya ujlinzi, Luiz pia atakwenda kufanya kazi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Brazil akina Dani Alves na Neymar katika mfumo ambao anauwezea na unampendezea.
    Msimu uliopita Barca iliteseka kutokana na Puyol kuwa nje kwa sababu ya maumivu, hivyo ikawalazimisha viungo Javier Mascherano au Alex Song kuhamia kwenye uinzi, hivyo Luiz kwa uwezo mkubwa hivi sasa ni mtu sahihi kwao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCELONA YAMTENGEA PAUNI MILIONI 30 DAVID LUIZ, LAKINI CHELSEA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top