• HABARI MPYA

    Monday, July 08, 2013

    MOURINHO ABADILI MFUMO WA UCHEZAJI, AACHANA NA KUPAKI BASI, ASEMA SASA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO

    IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 3:34 USIKU
    KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba yuko tayari kumaliza desturi ya kukandiwa juu ya mfumo wake wa uchezaji 'kupaki basi' kwa kutumia soka ya kushambulia, ambayo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich anataka.
    Kocha huyo Mreno, ambaye ameanza maandalizi ya msimu mpya wiki hii katika kipindi chake cha pili cha kufanya Chelsea, aliingia mzioni katika awamu yake ya kwanza akiwa na iPad.
    Mourinho alitaniana na Frank Lampard na Gary Cahill wakati akikinoa kikosi chake kipya huko Cobham mchana. 
    To be Frank: Some of the Chelsea players might be surprised to see their new boss taking sessions with an iPad
    Kuwa Frank: Baadhi ya nyota wa Chelsea wanaweza kuwa wamepagwa kumuona kocha wao mpya akiongoza mazoezi na iPad
    Welcome back, Jose: Frank Lampard and John Terry will be pleased to see the return of Mourinho to Chelsea
    Karibu tena, Jose: Frank Lampard na John Terry wanaweza kuwa wamefurahi kumuona Mourinho amerejea Chelsea
    Under instruction: The Portuguese speaks to Demba Ba and Gary Cahill while armed with an iPad
    Chini ya maelekezo: Mreno akizungumza na Demba Ba na Gary Cahill huku ameshika iPad
    New boys: Marco van Ginkel (left) and Andre Schurrle have been settling into life at Chelsea's training ground
    Vijana wapya: Marco van Ginkel (kushoto) na Andre Schurrle wameanza kazi Chelsea

    Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Inter Milan mtindo wake uchezaji wa kujihami zaidi ulizaa maswali mengi siku za nyuma, lakini sasa anataka kuimarisha timu na kuwavutia mashabiki kwa soka ya kushambulia.
    "Nataka kuwafanya mashabiki wa Chelsea wafurahi – kwa matokeo, kwa mtindo wetu wa uchezaji, kwa uwezo wetu na haiba nzuri ya timu,"amesema.
    "Wanatakiwa kujua kwamba, kuna matokeo ya aina tatu katika mechi – ambapo tunaweza kushinda, sare au kufungwa – lakini wakati wote tunajituma kwa kila kitu,".
    Beaming: Jose Mourinho has spoken of his desire to embark on a playing style to please the Chelsea fans
    Mabadiliko: Jose Mourinho amezungumzia kubadili mfumo wa uchezaji ili kuwafurahisha mashabiki Chelsea
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOURINHO ABADILI MFUMO WA UCHEZAJI, AACHANA NA KUPAKI BASI, ASEMA SASA NI MASHAMBULIZI MWANZO MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top