• HABARI MPYA

    Monday, July 08, 2013

    SPURS YAPAMBANA ILI BALE ASIONDOKE...SASA YAMTIA KWENYE MABANGO YA PROMOSHENI YA KLABU

    IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 3:16 USIKU
    MASHABIKI wa Tottenham wamepewa ahueni juu ya mustakabali wa Gareth Bale kama ataendelea kuitumikia klabu yao msimu ujao, baada ya mshambuliaji huyo nyota kutimika katika picha za mabango ya promosheni ya klabu kwa msimu ujao wa 2013/14.
    Na kulikuwa kuna habari nzuri zaidi, wakati Rais wa Real Madrid, Florentino Perez aliposema dili la kumhamishia Hispania 'mchawi' huyo wa Wales bado bichi kabisa.
    "Ni mchezaji mkubwa ambaye ni mali ya klabu ambayo tuna uhusiano nayo mzuri, lakini hatujatoa ofa yoyote,"alisema.
    Here for now: Gareth Bale (left) poses alongside Kyle Walker, Jan Vertonghen and Hugo Lloris
    Hapa kwa sasa: Gareth Bale (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake, Kyle Walker, Jan Vertonghen na Hugo Lloris

    Bale amerejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Spurs leo na klabu imeonyesha dhamira yake ya kubaki na mchezaji huyo aliyefunga mabao 26 msimu uliopita kwa kumtumia katika matangazo ya jezi mpya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SPURS YAPAMBANA ILI BALE ASIONDOKE...SASA YAMTIA KWENYE MABANGO YA PROMOSHENI YA KLABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top