IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 3:08 USIKU
MSHAMBULIAJI Arouna Kone amesaini Mkataba wa miaka mitatu na Everton kwa ada ya Pauni Milioni 5 kumfuata kocha wake wa zamani, Roberto Martinez aliyekuwa naye Wigan, kuhamia Goodison Park.
Martinez amefanikiwa kuungana na nyota wake huyo mwenye umri wa miaka 29, abaye alimfundisha Uwanja wa DW.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amepewa heshima ya kurejea chini ya Martinez kwa mara nyingine tena.
Mabao: Arouna Kone amejiunga na Everton kwa Mkataba wa miaka mitatu na ada ya Pauni Milioni 5
Washindi: Kone amekamilisha uhamisho wake kuungana na kocha mshindi wa Kombe la FA, Roberto Martinez klabu ya Everton
"Kwangu ni heshima kurejea kufanya kazi na kocha kwa mara nyingine tena," Kone aliiambia tovuti ya klabu hiyo. "Msimu uliopita amenisaidia kiasi kikubwa,"alisema.