IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 2:57 USIKU
KLABU ya Tottenham imepata pigo katika mpano wake wa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, baada ya David Villa kuchagua kujiunga na Atletico Madrid.
Mshambuliaji huyo wa Hispania amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Barcelona, na anahamia Jiji la Hispania kwa ada ya Pauni Milioni 4.5.
Spurs, na Arsenal pia mapema mwaka huu, zilijaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ahamie England.
Anabaki Hispania: David Villa amechagua kujiunga na Atletico Madrid licha ya kutakiwa na Spurs na Arsenal
"Makubaliano na kusajiliwa kwa Villa kama mchezaji mpya wa Atletico vitakamilishwa baada ya mchezaji kukamilisha zoezi la upimaji afya," imesema taarifa ya Atletico katika ukurasa wake wa Twitter.
Awali, iliripotiowa kwamba Barcelona ilitaka kuwatoa Thiago Alcantara na David Villa sambamba na kiasi fulani cha fedha Old Trafford ili wapewe Wayne Rooney akacheze Hispania.



Awali, iliripotiowa kwamba Barcelona ilitaka kuwatoa Thiago Alcantara na David Villa sambamba na kiasi fulani cha fedha Old Trafford ili wapewe Wayne Rooney akacheze Hispania.
Vigogo hao wa Katalunya wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji licha ya kwamba tayari wanaye Neymar waliyemsajili mwezi uliopita.
Rooney, ambaye aliishuhudia Fainali ya michuano ya Tenisi ya Wimbledon jana Andy Murray akitwaa taji upande wa wanaume, anakabiliwa na kiza juu ya mustakabali wake Manchester United na aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu.
Hajatulia: Lakini vigogo wa Katalunya, Barcelona wanamtaka Wayne Rooney kuongeza mtu wa nguvu katika safu yao ya ushambuliaji
Mlengwa: Dili la Rooney litafanya United imsaini Thiago Alcantara, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford
Arsenal na Chelsea bado wana matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England ahamie London, ingawa ukweli unabaki hilo litakuwa jambo gumu kwa United kuwauzia silaha wapinzani.
Rooney na David Moyes wamekwishazungumza juu ya mustakabali wake: wawili hao walikutana nyumbani kwa Rooney kabla hata wachezaji hawajarejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wiki iliyopita, na Mscotland huyo akaweka wazi katika Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari wiki iliyopita.
Kocha huyo mpya wa United anatarajiwa kutoa taarifa yake ya usajili baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson rasmi mapema mwezi huu.
Kocha mpya: David Moyes anataka kuweka alama yake United baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson
Na hiyo imelifanya gazeti la Sport la Hispania kuandika kwamba Rooney anaweza kutumika kuongeza ubora La Liga.
Taarifa katika gazeti hilo ilisema kuondoka kwa Thiago kwa kiasi cha Pauni Milioni 17 ni kama kunawezekana na zaidi katika dili hilo, Villa pia, mwenye thamani ya Pauni milioni 8.5 ataondoka Nou Camp akiwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake.
Pamoja na hayo, Pauni Milioni 4 taslimu ingeongezwa ili kufikisha tahamani ya Rooney, zaidi ya Pauni Milioni 30.