• HABARI MPYA

    Monday, July 08, 2013

    BARCELONA YAIPA MAN UNITED DAVID VILLA, THIAGO ALCANTARA NA MAMILIONI YA PAUNI, WAO WAPEWE ROONEY TU

    IMEWEKWA JULAI 8, 2013 SAA 11:37 JIONI
    KLABU ya Barcelona inataka kuwatoa Thiago Alcantara na David Villa sambamba na kiasi fulani cha fedha Old Trafford ili wapewe Wayne Rooney akacheze Hispania.
    Vigogo hao wa Katalunya wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji licha ya kwamba tayari wanaye Neymar waliyemsajili mwezi uliopita.
    Rooney, ambaye aliishuhudia Fainali ya michuano ya Tenisi ya Wimbledon jana Andy Murray akitwaa taji upande wa wanaume, anakabiliwa na kiza juu ya mustakabali wake Manchester United na aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu. 
    Unsettled: But Catalan giants Barcelona want Wayne Rooney to add to their firepower up front
    Hajatulia: Lakini vigogo wa Katalunya, Barcelona wanamtaka Wayne Rooney kuongeza mtu wa nguvu katika safu yao ya ushambuliaji
    Target: Any deal for Rooney could see United sign Thiago Alcantara, linked to Old Trafford this summer
    Mlengwa: Dili la Rooney litafanya United imsaini Thiago Alcantara, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia  Old Trafford
    Arsenal na Chelsea bado wana matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England ahamie London, ingawa ukweli unabaki hilo litakuwa jambo gumu kwa United kuwauzia silaha wapinzani.
    Rooney na David Moyes wamekwishazungumza juu ya mustakabali wake: wawili hao walikutana nyumbani kwa Rooney kabla hata wachezaji hawajarejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wiki iliyopita, na Mscotland huyo akaweka wazi katika Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari wiki iliyopita.
    Kocha huyo mpya wa United anatarajiwa kutoa taarifa yake ya usajili baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson rasmi mapema mwezi huu.
    New striker: United are also keen to include David Villa in the deal - who is also a target for Tottenham
    Mshambuliaji mpya: United pia itanufaika na David Villa katika dili hilo - ambaye pia anatakiwa na Tottenham
    New manager: David Moyes is aiming to stamp his mark on United after taking over from Sir Alex Ferguson
    Kocha mpya: David Moyes anataka kuweka alama yake  United baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson
    Na hiyo imelifanya gazeti la Sport la Hispania kuandika kwamba Rooney anaweza kutumika kuongeza ubora La Liga.
    Taarifa katika gazeti hilo imesema kuondoka kwa Thiago kwa kiasi cha Pauni Milioni 17 ni kama kunawezekana na zaidi katika dili hilo, Villa pia, mwenye thamani ya Pauni milioni 8.5 ataondoka Nou Camp akiwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake.
    Pamoja na hayo, Pauni Milioni 4 taslimu itaongezwa ili kufikisha tahamani ya Rooney, zaidi ya Pauni Milioni 30.
    Suited and booted: Rooney was in the Royal Box to watch Andy Murray win Wimbledon title on Sunday
    Suti na buti: Rooney alikuwa eneo la watu mashuhuri, maarufu kama Royal Box akiangalia Andy Murray akitwaa taji la Wimbledon jana
    Rooney
    Beki, na mchezaji wa zamani wa United, Gerard Pique alimpamba sana mchezaji mwenzake huyo wa zamani wiki iliyopita kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa mmoja wa wachezaji bora duniani akihamia Barca.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCELONA YAIPA MAN UNITED DAVID VILLA, THIAGO ALCANTARA NA MAMILIONI YA PAUNI, WAO WAPEWE ROONEY TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top