• HABARI MPYA

    Friday, August 16, 2013

    MOURINHO APANIA KUFANYA KITU KIMOJA 'BABU KUBWA' CHELSEA

    IMEWEKWA AGOSTI 16, 2013 SAA 7:55 MCHANA
    JOSE Mourinho ameapa kurudisha mshikamano Chelsea, baada ya msimu mbovu ambao ulichangiwa na Rafa Benitez kuchukua nafasi ya kipenzi cha mashabiki Roberto Di Matteo.
    The Blues iliingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kutimuliwa kwa kocha aliyeipa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Di Matteo na hata ubingwa wa Europa League haukutosha kumuokoa Benitez.
    Na mmiliki Roman Abramovich akamgeukia Mourinho kwa mara ya pili wakati wa kiangazi.
    Mreno huyo mwenye miaka 50 alinukuliwa na gazeti la The Sun akisema: “Nataka mashabiki wawe na sisi kama familia ya Blue – Familia ya Blue ambayo mwaka jana kuna wakati ilionekana kuvunjika.
    Confident: Chelsea boss Jose Mourinho
    Kujiamini: Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
    “Ninachotaka ni kuirudisha familia kuwa pamoja, hivyo nawataka watuunge mkono. Nataka wachezaji waungwe mkono, nawataka waiunge mkono Chelsea.
    “Nawata wawe na sisi kwenye nyakati nzuri na mbaya, kwenye hali ya baribi na ya joto, nyumani au ugenini, tunaposhinda na kufungwa.”
    Kufungwa siyo neno la kawaida kwa Mourinho na siyo kitu ambacho angependa kukiona.
    Historia yake kwenye klabu hiyo alipoifundisha kwa mara ya kwanza inavutia, alitwaa mataji sita katika misimu mitatu, ikiwemo taji la Ligi Kuu mara mbili mfululizo mwaka 2005 na 2006, Kombe la Ligi mara mbili, Kombe la FA na Ngao ya Jamii.
    Lakini Mourinho hana hofu na kurudi kwake Stamford Bridge baada ya kupata mafanikio Inter Milan na Real Madrid.
    Reviled: Even European successs could not make Rafa Benitez popular
    Alichukiwa: Mafanikio Ulaya hayakumfanya Rafa Benitez awe maarufu
    Popular: But Roberto Di Matteo was axed despite winning Champions League
    Staa: lakini Roberto Di Matteo alitimuliwa licha ya kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya
    “Ulichokifanya tayari kimeshafanyika, hakuna mtu anaweza kukifuta, hakuna mtu anaweza kuifuta historia yangu Chelsea.” Alisema Mourinho
    “Na ninaijua akili ya watu wa Chelsea. hawawezi kusahau nilichokifanya hapo kabla. Hawatasahau kwamba nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya klabu hii.
    “Napenda kuonekana kama kocha mpya Chelsea, nataka kupimwa kwa kile nitakachokifanya sasa. Nataka kufanya kazi hapa.
    “Rekodi yangu ni nzuri sana, nimeshinda vitu vingi sana katika sehemu mbali mbali, kila mashindano niliyotaka kushinda nilishinda.
    “Hivyo sina presha kama ile ambayo huwa wanakuwa nayo makocha wenye mafanikio madogo. Presha niliyonayo ni presha ya kuipigania klabu yangu.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MOURINHO APANIA KUFANYA KITU KIMOJA 'BABU KUBWA' CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top