• HABARI MPYA

    Thursday, October 02, 2014

    MAN UNITED WAPUMUA, FELLAINI AANZA KUPIGA 'MATIZI' KIKAMILIFU

    HATIMAYE Manchester United imepata habari njema kuhusu baa la majeruhi linalowakabili kwa sasa kufuatia kupona kwa Marouane Fellaini na kurejea mazoezini kikamilifu, huku Ander Herrera akielezea uwezekano wa kurejea kazini ndani ya siku moja.
    Fellaini na Herrera ni miongoni mwa wachezaji 10 majeruhi wa United ambaye amekuwa nje tangu mwanzoni mwa msimu, akisababisha mwanzo mgumu kwa kocha Louis van Gaal Old Trafford.
    Fellaini amekuwa nje ya Uwanja kwa wiki tano zilizopita tangu aumie enka ya mguu wake wa kushoto mazoezini baada ya kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Swansea. 

    Marouane Fellaini amerejea mazoezini kikamilifu baada ya kupona enka

    Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 27.5 kutoka Everton ameanza mazoezi kikamilifu na kikosi cha kwanza Uwanja wa Carrington wiki hii kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya timu yake ya zamani Uwanja wa Old Trafford Jumapili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED WAPUMUA, FELLAINI AANZA KUPIGA 'MATIZI' KIKAMILIFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top