• HABARI MPYA

    Thursday, October 02, 2014

    MBEYA CITY WAPATA UDHAMINI MWINGINE

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Mbeya City FC jana imeingia katika makubaliano na kampuni ya Coca Cola Kwanza ya udhamini utakaodumu kwa muda wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi 150,000,000.00
    Mkataba huo umegawanyika katika maeneo makubwa mawili ambayo ni vinywaji (Maji aina ya Dasani wakati wa mazoezi na mashindano, pamoja na vinywaji vingine kulingana na mahitaji ya klabu vitakavyokuwa na thamani ya shilingi Milioni 15) pamoja na fedha taslimu shilingi Milioni 60.

    “Tunaishukuru kampuni ya cocacola Kwanza kwa kuonesha imani hiyo kwetu na kuamua kufanya nasi kazi kwa kipindi hiki cha matazamio,”. 
    “Kampuni ya CocaCola ni kubwa kimataifa na haijawahi kudhamini klabu katika ukanda wetu huu wa Afrika zaidi ya kudhamini mashindano kadhaa,Hivyo tunajiona wenye bahati kuwa moja ya klabu chache kupafanya kazi na kampuni hii kubwa,”imesema taarifa ya Mbeya City.
    Taarifa MCC imesema kwamba Udhamini huo utaimarisha mahusiano ya kampuni na wananchi hasa wapenda michezo, pamoja na kuendelea kujenga imani ya kampuni hii katika tasnia ya michezo nchini.
    Mbeya City wamesema; “Kazi kubwa iliyopo mbele yetu kama klabu ni kuendelea kujenga imani hiyo ili fursa nyingi zaidi ziweze kutumiwa na wanamichezo wengine katika michezo mingine hapa nchini,”. Tayari Mbeya City inadhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Limited kupitia betri za RB.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY WAPATA UDHAMINI MWINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top