• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2015

    AZAM FC YAITAMANISHA SIMBA NAFASI YA PILI, YATOA SARE TENA 1-1 NA MTIBWA MANUNGU

    AZAM FC sasa inahitaji miujiza kutetea ubingwa, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
    Bao la Azam FC jioni ya leo limefungwa na kiungo Himid Mao Mkami, wakati la Mtibwa limefungwa na mshambuliaji mkongwe, Mussa Hassan Mgosi.
    Matokeo hayo sasa yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 38 baada ya kucheza mechi 20, sawa na vinara, Yanga SC wenye pointi 43.   

    Sare hii ya pili mfululizo kwa Azam FC, baada ya katikati ya wiki kutoka 1-1 pia na Mbeya City, rasmi inaanza kuitamanisha Simba SC kuwania nafasi ya pili.
    Simba SC ina pointi 35 baada ya kucheza mechi 21 na itakutana na Azam FC wiki ijayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAITAMANISHA SIMBA NAFASI YA PILI, YATOA SARE TENA 1-1 NA MTIBWA MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top