• HABARI MPYA

    Friday, April 10, 2015

    IPI NAFASI YA VAN PERSIE MANCHESTER UNITED KWA SASA?

    Na George Mganga, DAR ES SALAAM
    TUNAPOLITAJA jina la Robin Van Persie au tunapolizungumzia ni jina ambalo lilichukua uzito mkubwa hasa enzi za Sir Alex Ferguson katika msimu ambao aliifundisha kilabu hiyo huku mchezaji huyo akiibuka kama kinara na mpachika mabao aliyepata hadi tunzo ya mfungaji bora wa ligi ya Uingereza.
    Achilia mbali ufungaji bora alioupata bali pia alikuwa kama mchezaji tegemezi ambaye alikuwa akiamua matokeo ndani ya timu na pindi panapoonekana pengo au kukosekana kwake kulionesha mapungufu hasa katika nafasi ya ushambuliaji.
    Robin Van Magoli jina maarufu ambalo alibatizwa na Watanzania wengi tokea msimu wake wa mwisho akiwa na Arsenal kama kilabu mama kwake hadi sasa na pia alipotimkia Manchester united na kuwa mfungaji bora wa goli 26 ndani ya mechi 38 za ligi hiyo na kufikisha idadi ya vikombe 20 kitu kilichomfanya aendelee hadi kuitumia jezi yake iliyoandikwa namba 20 kama kielelezo cha kuendeleza furaha ya ubingwa huo kwa msimu uliofatia.
    Taarifa za hivi karibuni siku za nyuma uongozi na madaktaribwa timu hiyo uliripoti kuwa mchezaji amepatwa na majeraha hali ambayo ilimsababishia akae benchi kitu ambacho kilimsababishia aweze kukosa mechi kadhaa za ligi katika ambao bado United ilikuwa na matokeo ya kusuasua.
    Tukijaribu kuiangalia nafasi ya mchezaji huyo katika kikosi cha sasa cha timu hiyo ambacho kinaonekana kuimarika tofauti na ilivyokuwa hapo awali bado pengo lake halionekani katika timu hiyo.
    Kuumia kwa mchezaji huyo na kuwa sababu ya yeye kutokuwepo katika kikosi tumeona nafasi yake Wayne Rooney amekuwa akiitumia vizuri na amefanya vema mno siku hizi za usoni akiweza kufunga goli 4 katika mechi 5 za mwisho za ligi hiyo huko England akiwa kama Nahodha wa timu na akisaidia kuirejesha katika nafasi NNE bora.
    Majukumu ya Wayne Rooney ambayo alikuwa akiyatumia kabla hajaanza kuitumia nafasi ya Robin Van sasa yameingiliwa na Fellain ambaye amekuwa chachu kubwa na hata tegemeo pia katika timu hiyo.
    Fellain amekuwa kama kiungo mtengenezaji ambaye amekuwa akimiliki mpira na kutengeneza nafasi nzuri za magoli huku akielewana vizuri pia na washambuliaji wa mwisho na kufanya timu iungane vizuri pale mbele.
    Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu hiyo akicheza kama beki wakati huo Phill Neville anakuambia kuwa kwasasa hadhani kama Louis Van Gaal anaogopa kuacha majina makubwa katika benchi maana kikosi kina mwelekeo mzuri.
    "Nadhani Van Gaal ameamua kutuhakikishia msimu huu kuwa haogopi kabisa kuacha majina makubwa katika benchi" alisema wakati anaongea na mtandao wa Goal.com
    Van Persie enzi zake anaibeba Man United kwa mabao

    Sasa kipi kinachofuata?
    Hadi sasa kilabu ya Manchester united bado haijaonesha dalili yoyote ya kumuongezea mkataba mwingine mshambuliaji huyo ambaye mkataba alionao hivi sasa unamalizika msimu wa majira ya kiangazi mwaka huu.
    Takwimu za mchezaji huyo hadi sasa zinaonesha ameshacheza mechi 24 na akiwa amefunga magoli 10 tu pia ametengeneza nafasi 2 za kufunga magoli halikadhalika ana 2.7 katika mashuti aliyopiga langoni na pamoja na wastani wa 8.5 pasi alizopiga (pass accuracy) zake.
    Kupitia akaunti ya twitter taarifa zimeripoti ndani ya wiki hii siku ya jumanne kuwa mshambuliaji huyo yupo fiti kucheza mechi ijayo dhidi ya Manchester City ya Jumapili.
    Tunachokisubiri sasa kutoka kwa Mwalimu wake Louis Van Gaal kutuaminisha sisi wanamichezo kama atazidi kumtumia siju za usoni, kuamua kumuongezea mkataba kabla haujaisha katika msimu ujao wa majira ya joto, na kama mambo yakienda hadi basi atakuwa hana nafasi katika timu hiyo.

    (Mwandishi wa makala haya ni mpenzi na msomaji wa BIN ZUBEIRY ambaye anapatikana kwa namba +255 688 665 508)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IPI NAFASI YA VAN PERSIE MANCHESTER UNITED KWA SASA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top