NAHODHA wa zamani  wa Manchester United, Rio Ferdinand amesema anaamini kitendo cha kocha Louis van Gaal kumrudisha Wayne Rooney katika nafasi yake anayoimudu na kuipenda kucheza, ushambuliaji kimesaidia timu hiyo kurudi matawi ya juu.
Rio, anayemalizia soka yake QPR, ameandika katika safu yake ya gazeti la The Sun kuelekea mchezo baina ya mahasimu wa jiji la Manchester Jumapili, kwamba kitendo cha Rooney kuchezeshwa kama mshambuliaji kimeleta uhai.
Amemtaka kocha huyo Mholanzi, Van Gaal kuendelea kumtumia Nahodha huyo wa sasa wa United kama mshambuliaji kiongozi, huku pia akisema kurejea kwa majeruhi Ander Herrera, Marouane Fellaini na Michael Carrick pia kumeongeza uhai katika timu.
Rio Ferdiand (kulia) amesema Manchester United wapo vizuri hivi sasa baada ya Wayne Rooney kurejeshwa kwenye safu ya ushambuliaji
"Kurejea kwa Carrick wazi kumeleta msaada, lakini kumchezesha Wayne Rooney mbele ndiyo kila kitu,' Ameandika Ferdinand. "Wayne ni mfungaji wa mabao.Anashikilia rekodi ya mabao United,"ameongeza.
"Ukweli ni kwamba  United wanamuhitaji Rooney aliye fiti asimame pale mbele,".


.png)
0 comments:
Post a Comment