• HABARI MPYA

    Friday, April 10, 2015

    LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKIENDI HII

    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii katika viwanja sita tofauti nchini, viwanja vinne vikitimua vumbi kesho jumamosi, na michezo miwili kuchezwa siku ya jumapili.
    Jumamosi JKT Ruvu watakua wenyeji wa Coastal Union katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es salaam, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Coastal Union watakuwa wageni wa JKT Ruvu kesho Chamazi

    Timu ya Mtibwa Sugar watawakaribisha Azam FC kwenye uwanja wa Manungu-Turiani mjini Morogoro,nayo  Ndanda FC watakua wenyeji wa timu ya Tanzania Prisons mjini Mtwara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
    Ligi hiyo itaendelea siku ya jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Young Africans watawakaribisha timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, huku mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage wenyeji timu ya Stand United wakiwakaribisha maafande wa  timu ya Polisi Morogoro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA WIKIENDI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top