• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2015

    SIMBA SC YAJIPIGIA ‘TANI YAKE’ TOTO LA YANGA, YALICHAPA 3-0 KIRUMBA

    Na Alex Sanga, MWANZA
    SIMBA SC imeiadhibu Toto African ya Mwanza, tawi la mahasimu wao, Yanga SC mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
    Ikichezesha vijana wake kadhaa wa timu B, Simba SC inayofundishwa na Mserbia Goran Kopunovic iliipoteza kabisa uwanjani Toto iliyopanda tena Ligi Kuu chini ya kocha mzalendo, John Tegete licha ya kucheza nyumbani.
    Simba SC ilipata bao lake la kwanza kwanza dakika ya 25, mfungaji Said Issa aliyemalizia kona ya Ibrahim Twaha ‘Messi’.
    Kocha wa Simba SC leo amiongoza timu yake kuichapa Toto African 3-0 Kirumba

    Hadi mapumziko, Wekundu wa Msimbazi walikuwa mbele kwa bao 1-0 na kipindi cha pili, Issa Abdallah akafunga bao la pili dakika ya 49 na Dickson Amundo la tatu dakika ya 78.
    Kikosi cha Toto African kilikuwa; Erick Ngwengwe, Robert Magadula/Steven Kigocha dk51, Ladislaus Mbogo, Bahati Mwanga, Carlos Protas, Anthony Matogolo, Ismail Aidan/Mohammed Soud dk47, Emmanuel Swita, Japhet Vedastus/William Kigocha dk47, Hamim Tamim na Frank Sekure.
    Simba SC; Denis Richard/Peter Manyika dk46, Nassor Masoud, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Said Issa, Abdulaziz Makame/Dan Sserunkuma dk58, William Lucian ‘Gallas’/Hassan Isihaka dk58, Iddi Baraka, Abdallah Seseme/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk70, Elias Maguli, Ibrahim Twaha/Ibrahim Hajib dk70 na Issa Abdallah.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAJIPIGIA ‘TANI YAKE’ TOTO LA YANGA, YALICHAPA 3-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top