BAO la dakika ya 78 la beki Lusajo Elukaga Mwaikenda usiku wa Alhamisi limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa saba, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake sita.
0 comments:
Post a Comment