WENYEJI, Pamba Jiji wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na jirani zao, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijiji Mwanza.
Kiungo Mganda, Peter Lwasa alianza kuifungia Kagera Sugar dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji mzawa, George Mpole kuisawazishia Pamba Jiji dakika ya 76.
Kwa matokeo hayo, kila timu inafikisha pointi tano katika mchezo wa nane na kuendelea kufuatana nafasi ya 14 Kagera Sugar na 15 Pamba zikizidiana wastani wa mabao.
Ken Gold iliyocheza mechi saba ndio inashika mkia kwa pointi zake nne.
0 comments:
Post a Comment