WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Bao pekee la Namungo FC leo limefungwa na beki Ibrahim Abdallah Ali ‘Mkoko’ dakika ya 14 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi tisa katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya 11.
Kwa upande wao Pamba Jiji waliorejea Ligi Kuu msimu huu baada ya miaka 22 wanabaki na pointi zao tano za mechi 10 sasa nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment