MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Brazil na klabu ya Real Madrid ya Hispania, VinÃcius Junior ameshinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka ya 2024 ambayo alikabidhiwa na Rais wa Shirikisho hilo la Soka la Kimataifa, Gianni Infantino katika hafla iliyofanyika Jijini Doha nchini Qatar usiku wa jana.
Naye kiungo wa Kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Aitana Bonmatà ameshinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa Mwak aya FIFA kwa mara ya pili mfululizo.
Ukawa usiku mzuri pia kwa Mtaliano, Carlo Ancelotti aliyeshinda Tuzo ya Kocha Bora wa Kiume na kukabidhiwa na Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger.
WASHINDI WOTE WA TUZO ZA FIFA 2024:
•Mchezaji Bora wa Kike – Aitana BonmatÃ
•Mchezaji Bora wa Kiume – VinÃcius Junior
•Kipa Bora wa Kike – Alyssa Naeher
•Kipa Bora wa Kiume – Emiliano MartÃnez
•Kocha Bora wa Kike – Emma Hayes
•Kocha Bora wa Kiume – Carlo Ancelotti
•Tuzo ya Marta – Marta
•Tuzo ya Puskas - Alejandro Garnacho
KIKOSI BORA CHA WACHEZAJI 11:
Emiliano MartÃnez (Aston Villa/Argentina), Rúben Dias (Manchester City/Portugal), Dani Carvajal (Real Madrid/Spain), Antonio Rüdiger (Real Madrid/Germany), William Saliba (Arsenal/France), Jude Bellingham (Real Madrid/England), Rodri (Manchester City/Spain), Toni Kroos (Real Madrid/Germany), Erling Haaland (Manchester City/Norway), Lamine Yamal (Barcelona/Spain), VinÃcius Junior (Real Madrid/Brazil).
0 comments:
Post a Comment