Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Aboagye Gerson kutoka Ghana, leo anatarajiwa kuanza majaribio katika klabu ya Simba SC.
Simba SC imemleta mshambuliaji huyo kufanya majaribio, baada ya kuvutiwa na wasifu wake waliopewa na wakala wake.
BIN ZUBEIRY inafahamu Aboagye yupo Dar es Salaam tangu wiki iliyopita na ilishindikana kufanya majaribio mapema kwa sababu ya timu kuwa kwenye maandalizi ya Ligi Kuu.
Baada ya kumaliza kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam mwishoni mwa wiki, kocha wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic sasa yuko tayari kumuangalia mpachika mabao huyo wa Ghana mazoezini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wanataka kuboresha kikosi chao kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu.
“Mwalimu ametoa maoni yake juu ya aina ya wachezaji anaowataka, nasi tumeanza kulifanyia kazi hilo,”amesema Hans Poppe.
Aboagye mwenye umri wa miaka 26, anakuja kufanya majaribio Simba SC akitokea klabu ya Zakho ya Ligi Kuu ya Iraq.
“Kama mwalimu atavutiwa naye, basi tutafanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumsajili. Kwa sasa tumeongeza umakini katika usajili wetu, kuhakikisha hatukurupuki katika usajili,”amesema.

![]() |
Aboagye kushoto wakati anasajiliwa Zakho ya Iraq. Mshambuliaji huyo anaanza majaribio Simba leo |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wanataka kuboresha kikosi chao kwa kuongeza wachezaji wenye uzoefu.
“Mwalimu ametoa maoni yake juu ya aina ya wachezaji anaowataka, nasi tumeanza kulifanyia kazi hilo,”amesema Hans Poppe.
Aboagye mwenye umri wa miaka 26, anakuja kufanya majaribio Simba SC akitokea klabu ya Zakho ya Ligi Kuu ya Iraq.
“Kama mwalimu atavutiwa naye, basi tutafanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumsajili. Kwa sasa tumeongeza umakini katika usajili wetu, kuhakikisha hatukurupuki katika usajili,”amesema.
![]() |
Aboagye wa pili kushoto walioinama akiwa katika kikosi cha kwanza cha Zakho kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Iraq. Mchezaji huyo wa Ghana sasa anataka kuhamishia makali yake Msimbazi |
0 comments:
Post a Comment