• HABARI MPYA

    Tuesday, May 05, 2015

    BONGE LA ‘MIDO’ KAMA VIERA LATUA LEO ‘KUTAFUTA KAZI’ LIGI KUU YA BARA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa kimataifa wa Seirra Leone, Lansana Kamara (pichaani kushoto) anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam mchana wa leo kwa ajili ya kuja kusaka timu ya kuchezea nchini.
    Haijajulikana bado Kamara anakuja kufanya mipango ya kujiunga na timu gani, lakini ni Yanga SC ambao imeelezwa wanasaka kiungo kufuatia kuwapo wasiwasi wa Haruna Niyonzima kuondoka mwezi huu atakaopomaliza Mkataba wake.  
    Kwa mujibu wa wakala Mganda anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimaaifa (FIFA), Gibby Kalule ambaye ndiye amewaleta nchini wachezaji kama Kpah Sherman wa Yanga na Leonel Preux wa Azam, mchezaji huyo atatua Saa 8:00 mchana wa leo.
    Alipoulizwa anakwenda timu gani, Kalule alisema; “Mimi ni wakala ambaye nimekwishafanya kazi na klabu zote kubwa hapa Tanzania, naomba nisiseme kitu, naomba hiyo kazi niwaachie klabu waliyoomba waletewe huyu mchezaji,”.
    Lakini Kalule amesema kwamba hana shaka na uwezo wa Kamara ni kiungo bora ambaye popote alipocheza alifananishwa na Nahodha wa zamani wa Arsenal, Patrick Viera. 
    Kijana huyo mdogo mwenye umri wa miaka 22, atakuja Tanzania akitokea Sweden ambako amechezea klabu za Umea FC aliyojiunga nayo Januari 1, mwaka huu akitokea Vimmerby IF iliyomsajili Machi 12, mwaka jana.
    Awali ya hapo, Kamara alichezea pia Eskilstuna City FK tangu Jan 1, mwaka 2013 akitokea  Vimmerby IF, klabu yake ya kwanza nchini humo tangu aondokea kwao kwenda kutafuta maisha Ulaya.
    Kalule amesema Kamara ana uzoefu wa kuchezea timu ya taifa ya Sierra Leone katika mashindano makubwa na hana shaka ataisaidia timu ya Tanzania atakayojiunga nayo.
    “Ana umbo zuri, mrefu, ana nguvu na kijana mdogo, ambaye baada ya muda mfupi klabu inaweza kumuuza sehemu nyingine kwa dau zuri,”amesema Kalule. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BONGE LA ‘MIDO’ KAMA VIERA LATUA LEO ‘KUTAFUTA KAZI’ LIGI KUU YA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top