Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wanaingia kambini leo katika hoteli ya Valley View, Kariakoo, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:30 jioni utaambatana na sherehe za Yanga SC kukabidhiwa Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.
Pointi 55 zimetosha kwa Yanga SC kubeba taji la Ligi la Kuu baada ya mechi 24 tu, kwani haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote, hivyo mchezo wa kesho kwao ni wa kukamilisha ratiba.
Hata hivyo, Yanga SC hawatapenda wakabidhiwe Kombe wakitoka kufungwa- hivyo ndiyo maana wanaingia kambini kufanya maandalizi mazuri kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
Yanga SC wanaingia kambini siku moja tu baada ya kurejea kutoka Tunisia jana, ambako mwishoni mwa wiki walitupwa nje ya michuano ya Afrika na Etoile du Sahel kwa kufungwa bao 1-0 mjini Sousse.
Matokeo hayo yaliifanya Yanga SC ing’olewe kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Lakini kwa Azam FC waliokuwa mabingwa watetezi, mchezo huo ni muhimu kwao kushinda ili kujihakikishia nafasi ya pili waweze kucheza Kombe la Shirikisho mwakani.
Azam FC ina pointi 45 katika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 24, mbele ya Simba SC yenye pointi 44 za mechi 25.
Maana yake katika mechi mbili (dhidi ya Yanga na Mgambo wiki ijayo) zilizobaki wanahitaji kushinda moja ili kupata pointi 48, ambazo haziwezi kufikiwa na Simba SC.
Azam FC imezipiku zote Simba na Yanga kwa kucheza michuano ya Afrika mara tatu mfululizo, mara mbili Kombe la Shirikisho 2013 na 2014, wakati mwaka huu imecheza Ligi ya Mabingwa.
Yanga SC mwaka jana ilicheza Ligi ya Mabingwa na mwaka huu Kombe la Shirikisho, wakati Simba ilicheza michuano ya Afrika mara ya mwisho mwaka 2013, Ligi ya Mabingwa.
Bado timu hiyo ya bilionea Alhaj Sheikh Said Awadh Bakhresa na familia yake ipo katika nafasi nzuri ya kurudisha jina lake makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri mwishoni mwa mwaka.

0 comments:
Post a Comment